Tovuti ya gazeti la The Guardian imeandika siku ya Jumapili, ikinukuu taarifa ya Wizara ya Uhamiaji ya Israel, kwamba Yuan Yang na Abtisam Mohamed walipigwa marufuku kuingia 'Israel' kwa tuhuma za kupanga namna ya kunakili na kurekodi shughuli za vikosi vya usalama na kueneza chuki dhidi ya Waisrael.
The Guardian limeandika kuwa, wabunge hao wawili pamoja na wasaidizi wao, walikuwa wamesafiri kwa ndege kutoka mji wa Luton, Uingereza kuelekea Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy amesema katika taarifa: "kukamatwa na kuzuiwa kuingia wabunge wawili wa Uingereza waliokuwa wakisafiri kuelekea Israel wakiwa ni sehemu ya ujumbe wa bunge ni kitendo kisichokubalika, chenye madhara na cha kutia wasiwasi mno".
Lammy almeongezea kwa kusema: "Nimewaeleza wenzangu katika baraza la mawaziri la Israel kwamba hii sio njia ya kuamiliana na wabunge wa Uingereza. Inachofuatilia kwa karibu serikali ya Uingereza ni kurejea kwenye usitishaji vita na kufanyika mazungumzo ya kusimamisha umwagaji damu, kuachiliwa mateka na kuhitimisha mapigano huko Ghaza.
Ifahamike kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umechukua hatua ya kuwadhalilisha wabunge wa Uingereza kwa kuwakamata na kisha kuwarejesha nchini mwao pasi na kuwaruhusu kuingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) katika hali ambayo, serikali ya London ni mmoja wa waungaji mkono wakubwa zaidi wa kisiasa, kifedha na wa silaha wa utawala wa Kizayuni katika mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo haramu dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.../
342/
Your Comment